Mkuu wa Wilaya ya Ilala apongezwa
Mkuu wa wilaya ya Ilala bi Sophia Njema amepongezwa na wananchi mbalimbali hapa nchini kutokana na kitendo chake cha kishujaa cha kutuliza v...

Mkuu wa wilaya ya Ilala bi Sophia Njema amepongezwa na wananchi mbalimbali hapa nchini kutokana na kitendo chake cha kishujaa cha kutuliza vurugu zilizotokea pale Ukonga Dar es salaam.
Wakiongea na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti watu wengi kitendo kilichofanywa na mkuu wa Wilaya hiyo kuingilia kati vurugu hizo za kupigwa wanachi mitaani na wale wanaodaiwa askari wa jeshi la polisi ukonga.
Vurugu kubwa zimetokea katika maeneo hayo ambapo chanzo chake inadaiwa ni askari polisi wa kikosini hapo kupatikana akiwa ameuliwa na watu wasiojulikana kando na kambi hiyo, kitu kinachodaiwa kiliwafanya baadhi ya askari wenzie kuingia mitaani na kuanza kuwashambulia raia bila kujari kama wanahusika pia askari hao inadaiwa waliharibu mali za watu na kupora.
Baada ya wananchi kuchoshwa na vurugu hizo za wanaodaiwa askari raia walianzisha maandamano ya kupinga manyanyaso hayo, kitu kilichosambabisha mvumo wa vurugu hizo kuwa mkubwa, hatimae mkuu wa Wilaya hiyo kuingilia kati na kuwataka askari hao kuondoka mitaani jambo lililoisbua shangwa na nderemo kutoka kwa wananchi wrngi.