Pin It

Barrick wakubali kulipa

Juhudi za rais John Pombe Magufuli za kuyabana makampuni ya kuchimba dhahabu, zimezaa matunda baada ya kampuni ya uchimbaji madini ya Barric...

Juhudi za rais John Pombe Magufuli za kuyabana makampuni ya kuchimba dhahabu, zimezaa matunda baada ya kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kukubali kulipa Tsh bilioni mia saba 700.

Taarifa zilizopatikana kutoka Ikulu Dar es salaam kupitia matangazo ya moja kwa moja zimeeleza kuwa kampuni hiyo imekubali kulipa kiasi hicho cha fedha, pamoja na kiasi hicho cha pesa kampuni hiyo imekubari kurekebisha mkataba huo kwa kufanya biashara ya usawa wa nusu kwa nusu yaani 50%.

Mh rais baada ya kukerwa na wizi katika madini aliamua kuifumua mikataba ya madini pamoja na kuzuia usafirishaji wa mchanga wa madini (makinikia), baada ya hapo wamiriki wa Barrick/acasia walikuja nchini ambapo majadiriano yalianza baina ya pande mbili yaani Serikali pamoja na wachimbaji hao wa madini.

Mazungumzo hayo yalianza julai 31 mwaka huu na leo hitimisho limefika mwisho kwa kuweka makubariano kama nilivyoeleza hapo juu.,mafanikio hayo yamesifiwa na kada mbalimbali za watu hapa nchini.

Related

News 1983093530371229576

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Comments

Video ya Siku

item