Pin It

Rais Magufuli avunja mtandao

Rais Dk John Pombe Magufuli amevunjilia mbali mlolongo wa upatikanaji wa makaa ya mawe kwa ajili ya kiwanda cha saruji cha  Dangote uliokuwa...

Rais Dk John Pombe Magufuli amevunjilia mbali mlolongo wa upatikanaji wa makaa ya mawe kwa ajili ya kiwanda cha saruji cha  Dangote uliokuwa unakwamisha uzalishaji wa bidhaa hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa magari 580 ya kiwanda hicho ya kusafirisha saruji,uzinduzi huo ulifanyika kiwandani hapo, Dk Magufuli alisikitishwa na mlolongo uliokuwa unakikabili kiwanda hicho juu ya upatikanaji wa makaa ya mawe hivyo alimuagiza waziri wa  Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kuhakikisha ndani ya siku saba awe amempatia Dangote eneo lake atakalokuwa akichimba makaa ya mawe kwa ajiri ya kiwanda chake ,na kama ikibidi mengine atauza kwa watu wengine.

Vilevile mh Rais arimuagiza Waziri wa Nishati na Madini kuhakikisha anafikisha gesi katika kiwanda hicho mapema ili kufanya kusiwe na ukwamishaji wowote wa uzarishaji saruji kiwandani hapo.

Kwa upate wake Waziri profesa Muhongo alimuhakikishia mh Rais kuwa agizo lake atalitekereza ndani ya siku tano tu.

Related

Makala 8473917904576627061

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Comments

Video ya Siku

item