Pin It

Watu watatu wahofiwa kufa maji Kigamboni

Taarifa ambazo bado hazijazibitishwa, na jeshi la Polisi zinadai kuwa, watu watatu wamekufa maji jana jioni maeneo ya daraja jipya la Mwl Ny...

Taarifa ambazo bado hazijazibitishwa, na jeshi la Polisi zinadai kuwa, watu watatu wamekufa maji jana jioni maeneo ya daraja jipya la Mwl Nyerere Kigamboni, wakati walipokuwa wakivua kwa kutumia mtumbwi mdogo

Kwamujibu  wa bw Adani Amoni ambae anakaa maeneo karibu na eneo hilo  la tukio zinadai kuwa watu hao walipatwa na dhuruba kali ya upepo ambao ulisababisha mtumbwi wao kupinduka na watu watatu walifariki na mmoja kunusurika.

Taarifa hizo zinadai kuwa jeshi la Polisi hadi leo asubuhi lilikuwa linaendelea kutafuta maiti za wanaodaiwa kufa maji,hata hivyo juhudi za mwandishi wa habali hizi zakupata uthibitisho kutoka kwa kamanda wa Polisi kanda maalumu..ya Dar es salaam bw Simon Sirro hazikufanikiwa.

Yawapasa watutumiaji wa vyombo vya majini, kuwa na tahadhari hasa kipindi hiki ambapo upepo ni mkali.

Related

News 1374371101952497625

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Comments

Video ya Siku

item