Pin It

Majahazi yazuiwe kusafiri usiku

Miaka ya karibuni kumekuwa na wimbi la kuzama vyombo vya usafiri majini ikiwa ni  meli,boti pamoja na majahazi ikitu ambacho kimekuwa kikigh...

Miaka ya karibuni kumekuwa na wimbi la kuzama vyombo vya usafiri majini ikiwa ni  meli,boti pamoja na majahazi ikitu ambacho kimekuwa kikigharimu maisha ya watu na mali zao.

watu mbalimbali wameiomba Serikali ichukue hatua muhimu ili kuzuia hali hiyo mbaya inayorudisha nyuma maendeleo ya Taifa.

Hatua walizopendekeza watu zichukuliwe ni kuhakikisha kila chombo cha usafiri majini kiwe na dhana za kuokolea kama vile majaketi ya kumfanya mtu aelee majini,vifaa vya mawasiliano,semina elekezi juu ya matumizi ya dhana hizo
pamoja na hayo vyombo vyote vya kusafirisha watu vizuiwe kusafiri usiku.

Watu wamependekeza kuwa Serikali ichukue  hatua ya kuzuia usafirishaji watu usiku,kama ilivyokuwa kwa mabasi,ambapo Serikali ilizuia mabasi kusafiri usiku baada ya ajari kukithiri hasa nyakati za usiku.

Hivyo basi wamesema hata vyombo vya usafirishaji watu majini uzuiwe nyakati za usiku, kwasababu nyakati za mchana ni lahihisi hata namna ya uokozi.

Matukio mengi ya ajari majini yamekuwa yakitokea nyakati za usiku mfano mv Bukoba,mvSpice na hii ya usiku wa kuamkia  jana ya jahazi la mv Burudani iliyokuwa ikitokea Tanga kwenda Pemba iliyosababisha vifo vya watu kumi na mbili vilivyodhibitika mpaka sasa, pamoja na ajari nyingi nyinginezo.

Related

Makala 7781709549100687087

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Comments

Video ya Siku

item