Pin It

Askari polisi ajiua

Wahenga walisema mapenzi yanaua hawakukosea, hayo yamethiri kule Igunga na Rorya hivi karibuni kwa nyakati tofauti. Habari kutoka Igunga z...

Wahenga walisema mapenzi yanaua hawakukosea, hayo yamethiri kule Igunga na Rorya hivi karibuni kwa nyakati tofauti.

Habari kutoka Igunga zinaeleza kuwa askari polisi anayejurikana kwa jina la Geofray Mwenda (32)namba G.4185, wa kituo cha Igurubi wilaya ya Igunga, mkoa wa Tabora, amejiua kwa kujinyonga katika mti kutokana na vivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Hamis Issa alisema kuwa polisi huyo alijinyonga juma tano ya wiki hii baada ya kugundua kuwa mpenzi wake wa njea ya ndoa anabwana mwingine,awali polisi huyo alikuwa amemsafirisha mkewe kwenda kwao kusalimia.

 Habari kutoka mkoani Mara, wilaya ya Rorya, zimeeleza kuwa kijana aliyejurikana kwa jina la Lukas Jenge (24),mkaazi wa kijiji cha Muharango wilayani humo,zimeeleza kuwa, kijana huyo amejinyonga hivi karibuni  kwa kamba ya katani baada ya mama yake mzazi kumtaka amuache shemeji yake aliyemrithi baada ya kaka yake kufariki.

Related

Makala 2760927411195269397

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Comments

Video ya Siku

item