Pin It

Bibi kizee wakamatwa

Bibi kizee wa miaka 66 mkaazi wa kijiji cha Ngulyati mkoa wa Simiyu amekamatwa na polisi kwa kuwaunguza wajukuu zake. Kwa mjibu wa kamanda...

Bibi kizee wa miaka 66 mkaazi wa kijiji cha Ngulyati mkoa wa Simiyu amekamatwa na polisi kwa kuwaunguza wajukuu zake.

Kwa mjibu wa kamanda wa polisi wa mkoa huo tukio hilo limetokea mwezi huu katika kijiji hicho, ambapo watoto wawili mmoja anamiaka sita na mwingine anamiaka kumi na moja, waliunguzwa sehemu za makalio baada ya kushindwa kulinda mtama wa chakula ulioanikwa juani na bibi huyo jambo lililosababisha uliwe na kondoo.

Polisi inamshikilia bibi huyu kusubiri uchunguzi ukamilike ili aweze kupelekwa mahakamani.

Katika tukio lingine polisi mkoa wa Mwanza wanamshikilia Amina Hamis miaka 46 kwa kosa la kumlazimisha mtoto kula kinyesi.

Kwa mjibu wa kaimu kamanda wa mkoa huo Augustino Senga tukio hilo limetoa novemba 11katika jiji hilo ambapo mtoto ambaye hakutajwa jina lake kulazimishwa kula kinyesi alichojisaidia chooni bila kumwaga maji.
Majirani walitoa taarifa polis juu ya tukio hilo, ambao walimitia mbaroni mama huyo na sasa wanasubiri uchunguzi ukamilike ili wamfikishe mahakamani.

Related

News 974291261309744517

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Comments

Video ya Siku

item