Pin It

Moto wateketeza maduka Kigamboni

Moto ambao chanzo chake bado hakijajulikana, umeteketeza zaidi ya maduka 30 usiku wa kuamkia leo pale Ferry Kigamboni. Akizungumza na mwan...

Moto ambao chanzo chake bado hakijajulikana, umeteketeza zaidi ya maduka 30 usiku wa kuamkia leo pale Ferry Kigamboni.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mmoja wa wamiliki wa maduka hayo bw Hamad Kombo, alisema kuwa moto huo ulianza saa tano za usiku, nakwamba mmliliki wa jengo hilo aliwapigia simu watu wa fire , ambao walikuja wakiwa wamechelewa muda wa saa saba usiku huo.

Vilevile Bw Kombo alisikitishwa na kitendo cha (fire) jeshi la zima moto kutuma gari moja ambalo nalo liliishiwa maji. pamoja na hayo bw Kombo alisifu utendaji kazi wa jeshi la zimamoto kwa juhudi kubwa walizozifanya katika juhudi za kuzima moto huo

"Fire walipewa taarifa mapema ajabu walituma gari moja ingawa baadae walileta mengine tunaomba wawe na kituo kikubwa huku ikizingatiwa kigamboni inawatu wengi pia hivi sasa ni wilaya.

Kwa upande kiongozi wa jeshi la zima moto aliye kuwepo eneo la tukio Ass ambae pia ni kamand wa Temeke na Kigamboni afande Laizer Loshipay ,alisema kuwa taarifa waliziatazikiwa zimechelewa kupitia kwa Rpc wa Temeke, hivyo aliwataka wanachi utumia namba zao za matukio mbalimbali ambazo ni 114

Paja na hayo bw Loshipay alisema kuwa walijitahidi ndio maana hakuna majeruhi isitoshe walileta magari manne nama T673 DGL , ZT 0009,ZT 0014 ZT0030 aliongeza kuwa wapo katika mkakati wakujenga kituo kikubwa Kigamboni  kwani hivi sasa tukio likitokea kigamboni magari yanatoka mbali Ilala, Tazara ,na Lugaro.
.Picha mbalimbali za tukio la moto Kigamboni

Related

News 1995705587242790532

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Comments

Video ya Siku

item