Pin It

Serikali kupambana na wauza shisha

Mh Waziri mkuu Kasimu Majaliwa amemtaka mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ndugu Paulo makonda kuhakikisha anapamba na wauzaji na watumiaji wa ma...

Mh Waziri mkuu Kasimu Majaliwa amemtaka mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ndugu Paulo makonda kuhakikisha anapamba na wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya aina mbalimbali ikiwemo shisha.
Mh Waziri mkuu aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa uboreshaji wa miundombinu ya umeme mkoani Dar es salaam,mh Waziri mkuu alimtaka mkuu huyo wa mkoa ahakikishe anasimamia kikamilifu agizo alilolitoa kwa wakuu wa wilaya zilizopo katika mkoa wake,kuwa wapambane na wauzaji na watumiaji wa shisha.
Mh Waziri mkuu alisema endapo mkuu huyo wa mkoa asiposimamia ipasavyo atamwajibisha yeye.
Hayo yalitokana na kauli ya mkuu wa mkoa huo kuwatuhumu kamanda wa wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaamu Simon Sirro na kamanda wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni kamishina msaidizi Suzan Kaganda kuwa huenda wamehongwa na maajenti wa shisha.
Awali mkuu huyo wa mkoa alionyesha kushangazwa kuona utumiaji wa shiaha umerejea katika mkoa wake akahisi huenda viongozi hao wa vyombo vya usalamu huenda wamehongwa kwa kuwa hawaonyeshi udhati wa kupambana na tatizo hilo, ikizingatiwa kuwa kwa mjibu wake kuna maajenti wa shisha walimfuata ili wampatie hongo ya millioni hamsini kila mwezi hata hivyo alikataa hongo hiyo.

Related

Siasa 2399630151905777974

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Comments

Video ya Siku

item