Pin It

Rais apongezwa

Rais Dk John Pombe Magufuli,amepongezwa kutokana na hatua yake ya kuivunja bodi ya TRA kwa sababu ya kuchukua fedha za taasisi hiyo na kuzih...

Rais Dk John Pombe Magufuli,amepongezwa kutokana na hatua yake ya kuivunja bodi ya TRA kwa sababu ya kuchukua fedha za taasisi hiyo na kuzihifadhi katika mabenki matatu binafsi kwa muda maarumu ili kujipatia faida.

Wananchi mbalimbali waliozungumza na mwandishi wa habari hii wamepongeza uamzi huo wa Rais,ambapo wameonyesha masikitiko makubwa ikizingatiwa kuwa taasisi hiyo niya umma hivyo haipaswi viongozi wake kufanya maamuzi ya kinyemela tena kwa kificho.

"Unajua brother,kila mtu siku hizi analia kukosekana kwa pesa ukata kila kona kumbe kuna wajanja wachache wameficha pesa zetu"alilalamika nduguJafari Zuberi mkaazi wa Kigamboni.

Pia mmoja wa wafanyabiashara wakubwa hapa nchini ambae hakupenda kutajwa jina lake,aliunga mkono uamuzi wa mh Rais Magufuri kuwa umekuja wakati muafaka ambapo Taifa linahitaji fedha nyingi kwa matumizi mbalimbali,aliongeza kuwa wao wamekuwa wakienda hazina kuomba mikopo na kuambulia patupu,kumbe wajanja wamezificha fedha.

"Inasikitisha mno kila tukienda hazina kuomba mikopo hatupati kumbe wenzetu wanazizungusha pesa za Serikali,nikuambie kuwa mchezo huu upo kwa muda mrefu sana na unajurikana kwa baadhi ya viongozi, lakini hakuna kilichokuwa kinafanyika kwa wabadhirifu hao ikiwemo kuchukuliwa hatua kwa kuwa hata waliositahiki kuchukua hatua nao waligeuka kuwa wahujumu"alisikitika mfanyabiashara huyo.

Rais Magufuri ameamua na atafanikiwa kinachotakiwa ni kuungwa mkono na watu wote pamoja na vyombo vya dola kwani wao ndio waliopo katika kila sehemu wamsaidie mh Rais alisisitiza.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Comments

Video ya Siku

item