Pin It

Rais Magufuli apongezwa

Rais John Pombe Magufuli amepongezwa na watu mbalimbali kutokana na uamzi wake wa kuliagiza jeshi la wananchi Tanzania (JWT), kujenga ukuta ...

Rais John Pombe Magufuli amepongezwa na watu mbalimbali kutokana na uamzi wake wa kuliagiza jeshi la wananchi Tanzania (JWT), kujenga ukuta utakaozunguka eneo lote lenye madini ya tanzanite.

Akizungumza na wananchi wa Simanjiro mh rais alionyesha kusikitishwa na umasikini uliopo kwa wakazi hao huku wakiwa wamezungukwa na madini hayo yanayopatikana hapa nchini tu.

inasikitisha sana kwamba watu waliopewa madaraka hugeuka na kuwa wezi wa rasilimali za Taifa,angalia kama hapa hakuna hata ambulace sasa nitawaleteamimi alisema rais Magufuli.

Vilevile mh rais alisikitishwa kuona kuwa nchi ambazo hazina madini hayo ndizo zinaongoza kwa kuuza tanzanite Duniani'alitolea mfano moja ya nchi za Asia imeajiri watu wake wapatao laki sita kutokana na madini hayo.

maamuzi ya rais ya kujengwa kwa ukuta umepongezwa na watu mbalimbali,bw Joshua Athanas mkaazi wa Simanjiro alisema kuwa huyu ndiye rais tunalizishwa nae ataondoa wizi uliofanywa na watu wachache uliosababisha uangamazaji wa uchumi wa Taifa.

Related

Makala 5763323916752985548

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Comments

Video ya Siku

item