Mvua za bomoa barabara
Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha ,katika maeneo mbalimbali nchini ,zimesababisha madhara kadha wa kadha, ikiwa ni pamoja na kuhalibu miundo...

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha ,katika maeneo mbalimbali nchini ,zimesababisha madhara kadha wa kadha, ikiwa ni pamoja na kuhalibu miundo mbinu, kuharibu bidhaa, mazao pamoja na kukosesha makaazi baadhi ya watu.
Taarifa kutoka Tanga, zinaeleza kuwa mpaka sasa watu saba wamefariki kutokana na mvua hizo, barabara ya Tanga kuelekea Arusha imefunikwa na maporomoko ya udongo,na kusababisha mawasiliano ya barabara baina ya mikoa hiyo kukoma.
Vilevile inaelezwa kuwa barabara ya Bukoba kwenda Mwanza imetitia katika eneo la Kemondo na kufanya usafiri wa mikoa hiyo kuwa mubovu ,pia habari kutoka Zanzibar zinaeleza kuwa hali ni mbaya kwasababu baadhi ya barabara hazipitiki kutokana na kufunikwa na maji , isitishe baadhi ya shule zimefungwa kisiwani humo kutokana na kuzingirwa na maji
Hali ipo hivyo pia katika jiji la Dar es salaam pamoja na morog