Mizani isicheleweshe wasafiri.
Magari kupima katik mizani ni jambo jema kabisa, lakini kuna wakati inakuwa karaha. Kama nilivyosema awali magari kupima uzito kati mizani...

Magari kupima katik mizani ni jambo jema kabisa, lakini kuna wakati inakuwa karaha.
Kama nilivyosema awali magari kupima uzito kati mizani zetu ni muhimu mno, hasa katika kuwathibiti madereva wakorofi wanaozidisha uzito, kitu ni kibaya mno kwani ni moja ya sababu ya kuharibika barabara zetu zilizojenngwa kwa gharama kubwa .
Kwahiyo upimaji uzito wa magari sharti uendelee, lakini ni kitu kibaya sana kwa maofisa wapimaji katika mizani kuweka msururu wa magar huku wakijua watu waliomo katika magari hayo wengini wanaenda kujaribu kusaidia ndugu zao wagonjwa, wengine wanawahi manawahi misiba .
,Nawashauri hawa jamaa wanapoona mizani yao imezidiwa waruhusu baadhi ya magari yakapime mbele, badala ya kuyarundika sehemu moja nasema haya kutokana na nilichojionea hivi karibuni katika mizani ya Vigwaza mkoa wa Pwani
ambapo magari makumi kwa makumi yalikuwa yameweka msururu mrefu,bila maofisa wa upimaji kujari, sio vizuri hata kidogo mizani zipo kila kona waache umimi.