makala
Bondia kijana, Antony Joshua wa Uingereza amemshinda kwa k o bondia mkongwe wa Ukrain Wladimir Klischko katika raundi ya 11. Pambano hilo...

Bondia kijana,
Antony Joshua wa Uingereza amemshinda kwa k o bondia mkongwe wa Ukrain Wladimir Klischko katika raundi ya 11.
Pambano hilo lililofanyika katika uwanja wa Wembley uliosheni watazamaji elfu 90,pia lilitazamwa na matafa zaidi ya 140 ulimwenguni,lilikuwa ni pambano lakuvutia ambapo mabondia wote walionyeshana ujuzi wa hali ya juu.
Bondia Joshua alimdondo klischko ilipofika raundi ya tano, nakuamsha shangwe kwa mashabiki wake, hata hivyo Klishchko alimgeuzia kibao mpinzani wake katika raundi ya sita pale alipompelekea konde zito lililompekea kudondoka chini kama embe dodo.
Hata hivyo Joshua alisimama na kuendelea na pambano ambapo waliendelea kurushiana makonde ,ilipofika raundi ya kumi mambo yalianza kumuendea vibaya Klischko kwani alitandikwa makonde ya maana yaliyompeleka chini, ni katika raundi ya 11 bondia Joshua alionyesha umwamba wake kwa Klischko pale alipomdondosha mara mbili, hata hivyo Klischko alijaribu kuendelea na pambano ingawa alishindwa kuhimili makonde mazito ya Joshua,kitu kilichomfanya refa avunje pambano ili kumuokoa Klischko.