Serikali isihusishwe
Chama cha wananchi CUF kwa takribani mwaka mmoja sasa kipo katika mgogoro wa kiungozi jambo linalotishia kukiua chama hicho. Ni jambo la ka...

Chama cha wananchi CUF kwa takribani mwaka mmoja sasa kipo katika mgogoro wa kiungozi jambo linalotishia kukiua chama hicho.
Ni jambo la kawaida wakati mwingine vyama vya siasa kukumbwa na migogoro, hata CCM,imeshakumbwa na migogoro kama hiyo lakini kila chama huwa na njia zake za utatuzi,kinachosikitisha ni vyama vingine vinapokumbwa na migogoro yao ya kiuongozi hulaumu CCM au Serikali kuwa inahusika na migogoro hiyo.
Nasema inasikitisha kwa sababu CCMinapokumbwa na migogoro hutatua yenyewe bila kuhusisha vyama vingine mfano lahisi ni mgogoro uliotokea wakati wa kuteua mgombea urais mwaka jana2015 ambapo mmoja wa wagombea alihamia upinzani pale aliposhindwa kuteuliwa kutokana na kutokidhi vigezo vilivyowekwa na CCM.
Pamoja mmoja wa wagombea hao wa CCM kuhamia upinzani chama hicho hakikuwahi kuelekeza lawama katika vyama vya upinzani kilichofanya ni kurekebisha hali ya mambo ndani ya chama.
CUF wanamgogoro wao, waumalize wao bila kuelekeza lawama kwa Serikali wala chama tawala yaani CCM wakishindwa waache chama chao kife, waache lawama na waache kumwaga damu za Watanzania ambao nitegemeo la ujenzi wa Taifa.