Magufuli hoyeee
Nimeanza kwa hoyeee kwa Mh Rais Dk John Pombe Magufuli kwa sababu ya kazi anazozifanya zenye lengo jema la kuimalisha uchumi wa nchi yetu. ...

Nimeanza kwa hoyeee kwa Mh Rais Dk John Pombe Magufuli kwa sababu ya kazi anazozifanya zenye lengo jema la kuimalisha uchumi wa nchi yetu.
Awali baadhi ya watu walimbeza alipokuwa akitoa ahadi kwa wanchi, leo ni aibu yao kila kitu anachokizindua utekelezaji unaanza palepale, hakuna kulala huyo ndiye rais wa vitendo hakuna lelemama.
Alisema upanuzi wa barabara ya Morogoro leo inapitika, uwanja wa ndege Mwanza, na miradi mingine kibao juzi alikuwa katika uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa mwendo kasi, hela ya ujenzi inatoka katika mfuko wa Taifa.
Zote tunajua namna reli zilivyohujumiwa na kagenge ka watu wachache kwa manufaa yao, huku Taifa wakilihujumu waziwazi sasa mh Rais anamalizana nao Mwenyezi Mungu amlinde,Magufuli hoyeeeeee.