Tulimhimtaji Rais Magufuli
Kabla ya uchaguzi mkuu mwaka wa Tanzania wananchi wengi walikuwa wamechoka na mambo yalivyokuwa yakiendeshwa walihitaji mabadiliko. Watu w...

http://cmasele.blogspot.com/2016/12/tulimhimtaji-rais-magufuri.html
Kabla ya uchaguzi mkuu mwaka wa Tanzania wananchi wengi walikuwa wamechoka na mambo yalivyokuwa yakiendeshwa walihitaji mabadiliko.
Watu wengi kwa nyakati tofauti walisema walihitaji mabadiliko,kwamba walichoka na rushwa,walichoka na ubabaishaji,walihitaji Rais mwenye maamuzi,walihitaji vitendo,kwamba akisema hapana kweli iwe hapana.,ndio imaanishe hivyo kweli.
wananchi walichoka kwelikweli nchi iligeuka ikawa ya wapiga dili, ilikuwa ni semina zisizo na mashiko kila kona,makongamano,safari ndio usiseme viongozi wetu walipishana huku na kule ndani na nje ya nchi ilikuwa balaa,hakuna wa kukemea viongozi walikuwa wamekazana kweli kufuja kila walichoweza,ilikuwa kama mashindano ya kuhujumu Taifa.
Biashara haramu ilikuwa kama zimekubaliwa kimyakimya tembo waliuliwa hovyo hovyo faru, chui, simba,twiga walipakizwa bila woga vyura hawakusalimika mambo yalikuwa yamevurugika mno.
Biashara haramu ya madawa ya kulevya ilifanyika kwa mbwembwe, watu walisafirisha madawa ya kulevya sawa na unga wa sembe, wananchi wenye mapenzi mema na nchi yao walipiga kelele kupinga maovu mbalimbali,lakini wapi!, wakubwa walikuwa wameweka pamba masikioni.
Dk John Pombe Magufuri akiwa mtumishi wa umma yapo mengi aliyajua, yaliyokuwa ndani ya uwezo wake aliyakemea nakuyashughulikia,yapo mengi sana yaliyofanywa na Dk Magufuri akiwa naibu waziri na akiwa waziri ambayo kabla yalishindikana yeye aliyatatuanitayasema siku za usoni panapo majaariwa ya mwenyezi Mungu.
Dk Magufuri aliumia sana nadhana moyoni alisema ipo siku Mungu akimjaalia kuwa kiongozi wa nchi atayaweka sawa, wahenga walinena Mungu sio Athumani, lamgambo likalia jamani uchaguzi mkuu Magufuri akachukua fomu ndani ya CCM kimyakimya,hayawi hayawi ikawa chama kikampitisha.
Ulipowadia wakati wa kapeni alijua machungu ya wananchi kwa dhati, akaahidi mabadiliko na kwamba ataondoa maovu yaliyokuwayametamalaki, wapo waliomuamini wengine walisema hawezi kitu huyu.
Siku hazigandi uchaguzi ulifanyika Dk Magufuri alishinda, bila kuchelewa akaanza kushughurika na kupambana na maovu, akatuomba watanzania tumwombee, ukweli wananchi wema wamemuunga mkono.
Bahati mbaya watu wachache ama kwa akili zao au kwa kushawishiwa na wapenda maovu wameanza kupinga utawala wa Dk Magufuri, nawaomba sana watanzania wenzangu wavute kumbukumbu zao wajiulize Taifa lilikuwa kama halina mwenyewe ,Rais Magufuli yuko kazini anasafisha uozo uliokuwepo,tunatakiwa kumuunga mkono badala ya kujaribu kumrudisha nyuma.
Anachokifanya Rais ni sawa na kufanya usafi katika jumba lililokuwa limeterekezwa hakika akikung'uta vumbi litatimka watu watapaliwa lakini mwisho ya yote nyumba itakuwa safi na watu wataishi kwa amani huku wakivuta hewa safi Watanzania wenzangu tuvuteni subira neema inakuja, tusiyumbishwe na wale waliokuwa wamezoea kuibia Taifa.
Rais Dk Magufuri alipoahidi wakati wa kambeni kwamba anajua kinachofanywa na majizi na kwamba tukimchagua ataenda kufunga makufuri kumbe ni kweli tupu ndio maana anatia makufuri wanaopiga kelele ndio hao waliotufikisha hapa na bado,wisho watanyamaza asante Rais heshima ya Taifa sasa inarudi.